LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili ukiwemo wa ‘Dabi’ ya Mbeya kati ya Mbeya City na Ihefu katika uwanja wa Sokoine.
Mbeya City inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 5 baada ya michezo 5 wakati ihefu ipo mwisho wa msimamo wa ligi nafasi ya 16 ikiwa na pointi 1 baada ya michezo 5.
Katika mchezo wa pili Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa Polisi Tanzania katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kagera Sugar inashika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 2 baada ya michezo 5 wakati Polisi ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 2 pia baada ya idadi kama hiyo ya michezo.