Ngao ya jamii Wanawake Septemba 24

DAR ES SALAAM: NUSU fainali za michuano ya Ngao ya Jamii ikiwa ni kiashiria cha ufunguzi wa Ligi Kuu Wanawake Tanzania msimu mpya wa 2024/25 zitapigwa Septemba 24 hadi 27, uwanja wa KMC, Mwenge, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Wanawake Tanzania, michuano ya Ngao ya Jamii msimu huu itazikutanisha timu nne, bingwa wa ligi dhidi ya mshindi wa tatu na mshindi wa pili dhidi ya mshindi wa nne.
Timu ambazo zinaenda kucheza michuano hiyo ya Ngao ya Jamii kati ya Simba Queens dhidi Yanga Princess, JKT Queens dhidi ya Ceasiaa Queens, mshindi wa nusu fainali hiyo watacheza fainali na mshindi wa tatu Septemba 27.
Bingwa mtetezi wa Ngao ya Jamii ni Simba Queens iliyoitwaa katika fainali iliyopita Desemba 2023 dhidi ya JKT Queens kwa penati 5-4, ambaye alipata million tano (Mil.5) mshindi wa pili JKT Queens walipata Mil. 3.5, mshindi wa tatu Yanga Princess walipata Mil. 2.5.