Mwimbaji wa Injili atoa somo kwa wanandoa
NAIROBI: MSANII wa nyimbo za injili Mercy Masika ameandika somo la uvumilivu kwa wanandoa hasa wanapofikia hatua ya kutaka kuachana kutokana na kutofautiana kwao huku akitolea mfano wake hadi akatupa pete ya ndoa katika shamba lao la migomba alipokuwa ndani ya miaka sita ya ndoa.
Mercy amesema yeye na mume wake waliingia katika ugonvi uliosababisha wakatoleana maneno makali kiasi kwamba aliamua kutupa pete yake ya ndoa katika shamba lao la migomba huku mumewe, David Muguro, naye akifanya maamuzi yake.
“Mume wangu alikuwa akikabiliana na kufiwa na mama yake, matatizo ya kifedha na matatizo mengine ya familia. Tulikuwa tunapigana vita ambavyo hatukuelewa vilitoka wapi na ilituumiza sisi sote, “ameeleza.
“Nilisimama nje ya boma letu, nikiwa nimejifunga kwa mabishano makali na mume wangu. Sikumbuki hata maelezo, uzito tu wa mapambano ya kifedha, hisia zilizoongezeka, na hisia kwamba hatukuweza kukubaliana juu ya chochote, katika kuchanganyikiwa Mercy alisema:
“Bila kufikiria, Nilivua pete yangu ya ndoa, na kuitupa shambani nakumbuka nilipiga sana kelele nikijiuliza kama naweza kuishi bila yeye! Lakini nashukuru pete hiyo ilipatikana baada yam waka mmoja na ilionwa na msaidizi wa shamba letu hilo, Pete hiyo naendelea kuivaa kama ukumbusho wa umbali ambao tulikuwa tumetoka, kama ishara ya upendo wetu na agano la msamaha, unyenyekevu, na imani,” ameeleza.
Mercy alielezea mwaka wao wa sita wa ndoa kuwa ndio ulikuwa mgumu zaidi, huku kila kitu kikionekana kusambaratika. Kwa sasa wanamiaka 16 ya ndoa yao huku akiwataka wanandoa kumaloiza tatizo mapema linapotokea badala ya kulificha kwa muda mrefu huku akikiri kwamba ndoa si rahisi kama hutoshirikisha Imani yako.
Naye David Muguro, ambaye pia ni mhudumu wa injili, anasimamia kazi ya muziki ya Mercy katika siku yake ya kuzaliwa, aliandika ujumbe mzito:
“Siku ya kuzaliwa yenye furaha, mpenzi wangu. Kila siku na wewe ni baraka tele. Kwa sababu unamng’ang’ania Yesu, unakuwa bora zaidi. Asante kwa kuwa rafiki yangu bora, mchungaji binafsi, mshirika wa huduma, na mume wangu mzuri. Maisha huwa bora na wewe kila wakati.”