LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kufanyika Dar es Salaam na Morogoro.
Mtibwa Sugar inayoburuza mkia nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 8 baada ya michezo 16 itaikaribisha Dodoma Jiji iliyopo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 19 kwenye uwanja wa Manungu Complex, Turiani, Morogoro.
Nayo KMC inayoshika nafasi ya 5 ikiwa na pointi 23 baada ya michezo 17 itakuwa mgeni wa JKT Tanzania iliyopo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 17 baada ya michezo 16 kwenye uwanja wa Maj. Jen. Isamuhyo, Dar es Salaam.