Ligi Kuu

Dube mchezaji Bora, Hamdi Kocha bora 

MSHAMBULIAJI wa Yanga Prince Dube, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa mwaka 2024/25, huku Miloud Hamdi pia wa Yanga akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati za tuzo iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, Dube alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akiwashinda Aziz Ki wa Yanga na Selemani Bwenzi wa KenGold, alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Mchezaji huyo alitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo saba ambayo Yanga ilicheza mwezi huo na kufunga mabao matano na kuhusika na mengine matano kwa dakika 562 alizocheza. Yanga ilishinda michezo sita na kutoka sare mmoja.

Kwa upande wa Hamdi aliyeingia fainali katika mchakato huo na Fadlu Davids wa Simba na Fred Minziro wa Pamba Jiji, aliiongoza Yanga kushinda michezo minne na sare moja, ambapo kwa mwezi huo Yanga ilicheza michezo saba.

Kamati ya Tuzo pia,  imemchagua Meneja wa Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo uliopo Dar es Salaam Ashraf Omar, kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Februari kutokana na kufanya katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button