Ligi Kuu

Azam FC, Singida Black Stars mguu sawa

DAR ES SALAAM: MAKOCHA wa timu za Azam FC na Singida Black Stars, Rachid Taoussi na Ramadhani Nsanzurwimo wameweka wazi namna watakavyoingia katika mchezo utakaopigwa kesho Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi.

Makocha hao wameweka mbinu zao walipozungumza na waandishi wa habari leo Novemba 27 kuelekea mchezo huo.

Kocha mkuu wa Azam FC, Rashid Toussi amesema ameweka mipango sahihi ya kuhakikisha timu yake inapata alama tatu mbele ya singida black stars.

“Tumefanyia kazi kila eneo kwenye uwanja wa mazoezi kikubwa tutatanguliza nidhamu kwenye mchezo wa kesho tutimize lengo letu,” amesema.

Naye Kaimu Kocha wa Singida Black Stars, Ramadhani Nsanzurwimo amesema maandalizi yapo vizuri licha ya kutokea heka heka katika michezo mitatu iliyopita.

“Kocha (Patrick Aussems) ameondoka lakini falfasa ya timu ipo pale pale, tuna timu nzuri tumekuja Dar es Salaam kutafuta matokeo ya alama tatu na sio kutembea,” amesema.

Nsanzurwimo amesema lengo lao ni kufanya vizuri na kila mechi kwao ni fainali na wanahitaji kupata matokeo ambayo watawaweka katika ramani.

Related Articles

Back to top button