Filamu

Muigizaji wa Kenya Senje, afariki Dunia

NAIROBI: TASNIA ya filamu nchini Kenya inaomboleza kifo cha mwigizaji mahiri Eillen Otieno, almaarufu Senje.

Otieno, ambaye alitamba kwenye tasnia ya filamu kama vile Igiza, Shanga, na Black & Blue, amefariki kutokana na matatizo ya ugonjwa wa miguu.

Taarifa za kifo chake zimeshtua wengi, huku salamu na rambirambi zikimiminika kutoka kwa mashabiki na wafanyakazi wenzake.

“Tunapoomboleza kuondokewa na muigizaji huyu mpendwa, tukumbuke mchango wake kwa sinema ya Kenya na kupeleka rambirambi zetu kwa familia na marafiki zake,” waliandika baadhi ya waombolezaji waliokuwa wakimzungumzia marehemu Seche.

Seche anafariki baada ya wiki kadhaa tasnia ya burudani Kenya kukumbwa na msiba mwingine wa mwanamahudhuri mtandaoni wakike kufariki dunia kutokana na maradhi.

Related Articles

Back to top button