Cruise, ‘Mission Impossible’ gumzo Tamasha la Cannes

CANNES: MCHEZA filamu Tom Cruise anajiandaa kurudi katika Tamasha la filamu la Cannes linalofanyika kila mwaka nchini Ufaransa akiwa na filamu yake ya ‘Mission Impossible The Final Reckoning’.
Filamu hiyo, iliyoongozwa na Christopher McQuarrie, itaoneshwa kwa mara ya kwanza Mei 14, kabla ya kutolewa huko India.
‘Mission: Impossible The Final Reckoning’, iliyoigizwa na Tom Cruise, itakuwa na onesho lake la kwanza la dunia katika Tamasha la Filamu la Cannes mnamo Mei 14 mwaka huu.
Filamu hiyo itaoneshwa bila ushindani, huku Cruise na muongozaji na mwandishi Christopher McQuarrie akithibitishwa kuhudhuria tamasha hilo.
Hii itaashiria kurejea kwa Cruise kwenye zulia jekundu la Cannes, akisindikizwa na waigizaji mbalimbali wakiwemo wanaoonekana katika Trela la filamu hiyo, iliyotolewa Jumatatu.
Filamu hiyo ni ya saba katika mfululizo na inatarajiwa kuhitimisha safu ya hadithi ya mhusika Cruise, Ethan Hunt.
Filamu hiyo itatolewa katika kumbi za sinema nchini India mnamo Mei 23 kwa Kiingereza, Kihindi, Kitamil na Kitelugu, ikijumuisha maonesho ya IMAX.