BurudaniFilamuMuziki

Mama Wema: sipendi ,maisha anayoishi Wema

DSM: Mama mzazi wa mrembo wa Filamu Wema Sepetu, Mariam Sepetu amemtaka mpenzi wa  Wema,Osca Lelo ‘Whozu’ kwenda kujitambulisha nyumbani kwake sio kujianika mitandaoni bila idhini za wazazi.

Akizungumza kwenye sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Wema Sepetu nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaam, Mama Wema amesema  Wema hamsikilizi.

“Hakuna mzazi anaependa kuona watoto wanaishi kama wanavyoishi binafsi sipendi kuona mwanaume yoyote anaishi kwa mwanamke lazima uonyeshe kuwa mwanaume, kama mnakaa kwa makubaliano nendeni kwa wazazi mjitambulishe, kwa mzazi yoyote hawezi kufurahia kinachofanyika.”

“Sipendi kumuona mwanangu au mtoto wa mtu yoyote anaishi na mwanaume bila baraka za wazazi ni muhimu sana hapo mnaonyesha jinsi gani hamna heshima kwa wazazi wenu ,fateni taratibu za mila na desturi sio kuanikana huko mitandaoni mnadhalilisha familia zenu.”

“Sipendi kumtembelea Wema nyumbani kwake kwa sababu anaishi na mtua mbae hajaja kujitambulisha kwangu, anaye mama japo baba yake katangulia mbele za haki anahitaji heshima za kufata wazazi.”amesema Mama Wema Sepetu.

Related Articles

Back to top button