Muigizaji India atoa chozi katika mazishi ya baba yake

MUMBAI: MUIGIZAJI wa filamu za India, Mannara amemuaga baba yake, Raman Rai Handa, huku akibubujikwa na machozi, leo Jumatano, Juni 18 katika ibada ya mwisho zilifanyika Mumbai nchini India.
Wakati video kadhaa za ibada ya mwisho ya Handa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii, video mpya inamwonesha Mannara akilia bila kufarijiwa na kuvunjika moyo wakati wa mazishi huku muigizaji huyo akionekana akimkumbatia dadake, Mitali Handa, katika kipindi hiki kigumu.
Baba ya Mannara Chopra alifariki dunia Juni 16. Alikuwa na umri wa miaka 72. “Kwa masikitiko makubwa na huzuni tunaarifu kifo cha kuhuzunisha cha baba yetu mpendwa ambaye alituacha kwenda kwenye makao yake ya mbinguni mnamo 06/16/2025. Alikuwa nguzo ya nguvu kwa familia yetu.”
Mannara hakuwa Mumbai wakati wa kifo cha baba yake. Walakini, alirudi mara moja kwa ajili ya maombolezo. Muigizaji huyo alionekana kwenye uwanja wa ndege wa Mumbai akiwa na dadake, Mitali, na alionekana mwenye huzuni sana.