Alia Bhatt: Awatisha mastaa wa filamu Bollywood
MUMBAI: MUIGIZAJI anayefanya vizuri katika soko la filamu la India, Bollywood, Alia Bhatt amesema wakati wake wa kushindana na wasanii wakubwa wa filamu nchini India umefika.
Bhatt amesema hayo baada ya kuachia kava la filamu yake mpya inayoitwa ‘Jigra’ ambayo amemshirikisha muigizaji anayefanya vizuri katika filamu za India, Vedang Raina
Kwa mujibu wa Alia Bhatt na Vedang Raina filamu ya ‘Jigra’ inatarajiwa kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema Oktoba 11, 2024, huku video ya awali ya tangazo la filamu hiyo ‘teaser’ ikitarajiwa kuachiwa Septemba 8, 2024 huku maandalizi ya uzinduzi wa filamu hiyo yakiendelea kwa kasi.
Alia alisema ‘Jigra’ imeongozwa na Vasan Bala na imetayarishwa kwa ushirikiano na Karan Johar’s Dharma Productions na Eternal Sunshine Productions ya Alia Bhatt.
Kabla ya onyesho la kwanza la filamu hiyo, watengenezaji filamu wamekuwa wakitoa maoni yao huku wengi wao wakimpongeza msanii huyo kwa kuamua kufanya sanaa yenye ushindani kwa kuleta filamu hiyo inayotarajiwa kufanya vizuri katika soko la filamu nchini India.
Kava la Filamu hiyo inamuonyesha muhusika mkuu Alia akiwa katika hali ya utayari kwa vita, tayari kukabiliana na changamoto zoyote atakazokutana nazo katika mazingira aliyopo.
Anaonekana akiwa amevalia shati jeupe na bluu lenye mistari milia na suruali nyeusi, na nywele zake fupi na mwonekano wake wa utayari kwa vita ukivutia wengi walilotazama kava la filamu hiyo.