Nyumbani

Pluijm kusafiria kivuli cha uchovu wa Yanga

KOCHA wa Singida Big Stars, Hans Pluijm amesema uchovu wa safari ya wapinzani wao Yanga utawasaidia kupata ushindi katika mchezo wa Nusu Faianali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) uliopangwa kuchezwa Jumapili hii Uwanja wa Liti mkoani Singida.

Akizungumza na HabariLEO, kocha huyo amesema hawapo tayari kufungwa mara tatu na timu moja hivyo wamejipanga kuhakikisha wanacheza kwa kujitoa zaidi ili kupata ushindi na kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

“Nimezungumza na wachezaji wangu na kuwaambia kama kweli tunataka kushiriki mashindano ya kimataifa lazima tuanze kwa kuifunga Yanga Jumapili na hilo litatimia kwa kila mtu kutimiza jukumu lake kwa asilimia 100 nafurahi kila mmoja amenihakikisha hilo,” amesema Pluijm.

Related Articles

Back to top button