Nyumbani

Tanzania, Japan kuendeleza michezo

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo itaendelea kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Japan (JICA) katika sekta ya michezo nchini ili kuendelea kutoa ajira kwa watu wengi zaidi hatua inayosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Saidi Yakubu amesema hayo jijini Dodoma leo wakati wa kikao chake na Mtaalamu wa michezo wa JICA Dkt. Shiraishi Tomoya.

“Uwepo wako hapa nchini utasaidia wananchi kuongeza hamasa ya michezo na watu wengi wakishiriki watakwepa magonjwa yasiyoambukiza,” amesema Yakubu.

Kwa upande wake Dkt. Shiraishi Tomoya amesema katika miaka 10 ijayo michezo itakuwa sehemu ya jamii ambapo watu wote watashiriki na kuimarisha afya zao.

Dkt. Tomoya ni mtaalamu na mshauri wa michezo na maendeleo na atakuwepo nchini kufanya kazi katika Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa muda wa miaka mitatu hadi 2027.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button