Filamu

Mtayarishaji Lynda Obst afariki akiwa na miaka 74

LOS ANGELES: MTAYARISHAJI filamu aliyefanya vizuri kwenye filamu pendwa ya ‘Sleepless in Seattle’, Lynda Obst amefariki akiwa na umri wa miaka 74.

Oly aliiambia The Hollywood Reporter kwamba Obst amefariki nyumbani kwake Los Angeles akiwa amezungukwa na wapendwa wake, mwanawe na meneja wake.

Filamu alizowahi kuzizalisha mtayarishaji huyo ni pamoja na ‘Contact’, ‘Flashdance’, ‘The Fisher King,’ ‘Adventures in Babysitting’, ‘How to Lose a Guy in 10 Days’ na ‘Interstellar’.

“Mama yangu alikuwa mfuatiliaji na mtetezi mkubwa wa wanawake. Pia, alikuwa mama wa ajabu, dada na rafiki mkubwa,

“Julie na mimi tunashukuru sana kwamba alikuwa mama yangu na kwamba binti zangu walimpata nyanya shupavu lakini sasa tumemkosa.” Oly alisema katika taarifa yake.

Naye Kaka wa Obst, Rick Rosen, aliyewahi kufanya vizuri katika TV, amesema: “Familia yetu inajivunia sana kazi aliyokuwa nayo na mfano wa kuigwa kwa wanawake katika tasnia, lakini zaidi ya hayo, tutamkumbuka daima.

upendo wa ajabu wa familia yetu. Sikuzote alikuwa na furaha zaidi alipokuwa karibu na familia.”

“Obst alipambana na ugonjwa sugu wa mapafu, unaojulikana zaidi kama COPD au wakati wa uhai wake alitutania kwamba ugonjwa huo ulitoboa mapafu yake na asingeweza kupona,” Alisema Rosen.

Related Articles

Back to top button