
MUMBAI: WAZIRI Mkuu wa India Narendra Modi, Mawaziri wa Muungano, wabunge, muigizaji Vicky Kaushal, na waigizaji wengine wanatarajiwa kuhudhuria onesho maalum la filamu ya Chhaava litakalofanyika bungeni nchini India.
Filamu hiyo ya muigizaji Vicky Kaushal, inatarajiwa kuoneshwa katika jengo la Maktaba ya Bunge kwenye Ukumbi wa Balayogi siku ya Alhamisi, Machi 27.
Vicky Kaushal amecheza kama Chhatrapati Sambhaji Maharaj katika filamu hiyo. Alikuwa mtoto wa Chhatrapati Shivaji Maharaj, mwanzilishi wa Dola ya Maratha.
Katika hafla ya uzinduzi wa 98 ya Akhil Bharatiya Marathi Sahitya Sammelan (ABMSS) mnamo Februari, Waziri Mkuu Modi alisifu filamu hiyo ya Chhaava, akiita filamu ya kihistoria na Vicky Kaushal alimshukuru Waziri Mkuu huyo kwa kuisifu filamu hiyo.
Filamu ya Chhaava imetayarishwa na Maddock Films, na imewashirikisha waigizaji wengi wakiwemo Akshaye Khanna, Diana Penty, Vineet Kumar Singh, na Ashutosh Rana.
Filamu hiyo imeongozwa na Laxman Utekar, na inahusu hadithi ya jinsi Sambhaji Maharaj alivyokuwa jasiri katika kutetea imani na nchi yake. Filamu hiyo ilianza kuonyeshwa sokoni Februari 14 mwaka huu. Kufikia sasa, filamu hiyo imepata zaidi ya randi 700 crore, kulingana na Sacnilk.com.
Filamu hiyo imesharipotiwa polisi ikidaiwa kuibwa mtandaoni, na zaidi ya channel 1,818 zimeonekana kutumia filamu hiyo katika mitandao yao bila kibali, kulingana na shirika la habari la ANI.