Filamu

Michael Jordan arudi kama muongozaji filamu

NEWYORK: BAADA ya kutamba sana katika uigizaji wa filamu mbalimbali muigizaji Michael B. Jordan amerejea katika uongozaji wa filamu na ataanza kuongoza filamu ya ‘The Thomas Crown Affair’.

Filamu hiyo itakayoongozwa na Jordan itakayosimamiwa na studio ya Amazon MGM, kwa kushirikiana na Elizabeth Raposo kupitia kampuni yake ya Outlier Society.

Jordan amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na kuwa nyota katika toleo jipya la ‘The Thomas Crown Affair’ kwa miaka kadhaa na sasa ameonekana kuwa muongozaji filamu lakini pia atakuwa muigizaji wa filamu hiyo.

Katika filamu atakayoiongoza Jordani awali iliigizwa na Pierce Brosnan na Rene Russo mwaka 1999 na pia ilifanywa na Steve McQueen na Faye Dunaway mwaka 1968.

Filamu hiyo inaeleza mtu tajiri anayedhani kuwa alitoroka kwa wizi wa gharama kubwa, lakini anajitokeza dhidi ya mwanamke anayechunguza uhalifu wake.

Filamu hiyo inaonyesha pia mnamo mwaka 1968, McQueen ambaye ni mtendaji mkuu wa benki anayevutia anapigana kiakili na Dunaway, mpelelezi wa bima anayechunguza shughuli zake zisizo halali.

Jordan pia ana miradi kadhaa katika kazi zake lakini pia amemaliza utayarishaji wa filamu yake ya ‘Secret of Vampire’ na ‘I Am Legend 2’ inayosimamiwa na Steven Caple Jr.

Related Articles

Back to top button