Soka La Ufukweni

Mtanzania awania Tuzo ya mchezaji Bora Duniani

DAR ES SALAAM: NAHODHA wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, Jaruph Juma amechaguliwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowania Tuzo ya mchezaji bora Duniani 2024.

Jaruph alisajiliwa na klabu ya Ain Diab ya nchini Morocco inayoshiriki Ligi Kubwa ya mchezo wa soka la Ufukweni kwa kusaidia timu hiyo kufanya vizuri kwa msimu uliopita baada ya kuonesha kiwango kizuri kwenye timu ya Taifa ya Tanzania.

Nyota huyo wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania akicheza nafasi ya ushambuliaji amekuwa mtanzania wa kwanza katika michuano hiyo kuingia kinyanganyiro cha kuwania tuzo hiyo akishindanishwa na wachezaji mbalimbali kutoka bara la ulaya.

Baadhi ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ni Jaruph (Tanzania), Aaron Clarke ni nahodha wa timu ya soka ya ufukweni ya Uingereza, Amund Haalnd kutoka timu ya Taifa ya Norway, Ahmed Al Hamami anacheza Saud Arabia na Antonio Chavez (Marekani).

Related Articles

Back to top button