Michezo MingineSoka La Ufukweni

Usajili soka la ufukweni waanza leo

DIRISHA la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya Soka la Ufukweni(BSSL2023) limefunguliwa leo na litafungwa Mei 3, 2023.

Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema klabu zote zinakumbushwa kufanya usajili kwa wakati kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo.

“Kama kuna changamoto yoyote wasiliana na ofisa wa dawati la mpira wa miguu wa ufukweni wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF),” imesema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa shirikisho hilo hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha la usajili kufungwa.

Related Articles

Back to top button