Ligi Kuu

Kocha ken Gold aifungia kazi safu ya ulinzi

KOCHA Mkuu wa Ken Gold, Omary Kapilima amesema bado ana kazi ya kufanya katika safu ya ulinzi ambayo imekuwa ikiruhusu bao kila mechi.

Omary Kapilima amekabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi cha timu hiyo akichukuwa nafasi ya Jumanne Chale aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo na kufungishwa virago vyake.

Amesema licha ya kutengeneza nafasi na kuzitumia vizuri lakini wanapata wakati mgumu wa kulinda lango lao kwa kuruhusu bao katika kila mechi ambazo wamecheza.

“Mara ya kwanza tulikuwa tunatengeneza nafasi lakini tunashindwa kufunga lakini sasa hivi tumeweza kufunga, kazi ipo kwenye safu ya ulinzi tumekuwa tukiruhusu mabao kwa kila mechi, hili tunatakiwa kufanyia kazi,”  amesema Kapilima.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button