Ligi Kuu

Simba hadi raha!

ZANZIBAR: Mabingwa wa zamani wa kandanda la Tanzania, SIMBA wamepanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Azam FC, mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar

Mabao ya Simba kweye mchezo huo yalifungwa na Leonel Ateba dakika ya 15 kwa shuti ikiwa pasi kutoka kwa Jean Ahoua.

Simba waliongeza la pili lililofungwa na Fabrice Ngoma kwa kichwa dakika ya 47 ukiwa mpira uliochezwa na kipa wa Azam FC, Mohammed Mustafa baada kuokoa kichwa cha Kibu  Denis.

Kwa ushindi huo Simba inapanda hadi nafasi ya tatu kutoka Sita akikusanya pointi tisa baada ya michezo mitatu na ikimshusha Azam FC mwenye pointi 8 na baada ya michezo mitano ya ligi hiyo

Related Articles

Back to top button