Masumbwi

Mfaume ataka pambano la Oscar,Tony lirudiwe

DAR ES SALAAM: BONDIA wa ngumi za kulipwa Mfaume Mfaume ameomba pambano la Oscar Richard na Tony Rashid lirudiwe kutafuta uhalali wa mshindi.

Kwa mujibu wa Mfaume, mpaka leo hawaamini bondia wao Oscar alipigwaje na Tony kwa kuwa ni mtu mwenye uwezo kuliko mpinzani wake.

Katika pambano lililofanyika Juni mwaka huu Oscar aliyeko chini ya Nakoz Gym kwa Mfaume alipigwa kwa pointi hivyo, wanatamani liandaliwe pambano lingine kulipiza kisasi.

Akizungumza na SpotiLeo Mfaume amesema:”muda wowote, saa yoyote tunahitaji pambano na yule jamaa yaani Tony Rashid tukapoteza kwa pointi,

“Tunakubali kwamba katika michezo siku zote kuna kushinda, kutoka sare na kupoteza, tunaheshimu maamuzi ya majaji. Kama majaji walimpa ushindi yule tunaomba mechi ya marudiano tuko tayari,”amesema.

Amesema hata kama ni kesho wanaamini bondia wao Oscar anaweza kushinda kutokana na kuimarika na kuwahakikishia mashabiki wa ngumi kuwa Tony hatomaliza pambano hilo.

Related Articles

Back to top button