Marmoush, Ederson wazengea Etihad

MANCHESTER, Uingereza: Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England(EPL), Manchester City wanawania saini ya Mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Omar Marmoush na kiungo wa Atalanta Mbrazil Ederson Jose dos Santos da Silva maarufu Ederson.
Gazeti la the Sun la England linaripoti kuwa meneja wa Manchester city Pep Guardiola amewasilisha majina ya wachezaji hao ili wasajiliwe dirisha hili la Januari kuimarisha kikosi chake ambacho kipo unga kwa sasa.
Inaelezwa kuwa Matajiri wa Etihad wako tayari kuvunja benki ili kupata saini ya Marmoush kuimarisha eneo la ushambuliaji huku Ederson akitazamiwa kuja kupoza machungu ya kumkosa rodri.
Marmoush mwenye magoli 18 katika mchezo 24 aliyocheza anahusishwa pia na Washika mitutu wa jiji la London Arsenal na vinara wa ligi Liverpool.