EPL

Haaland, Palmer, Raya na Hurzeler waula PL Agosti

LONDON: Shambuliaji hatari la mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester city Erling Haaland ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa ligi hiyo.

Erling Haaland anashinda tuzo yake ya tatu ya uchezaji bora wa mwezi baada ya kuanza kwa kishindo ligi kuu nchini England akifunga hattrick 2 katika mechi 3 alizocheza.

Tuzo ya meneja bora wa August imeenda kwa Meneja wa Brighton and Hove Albion Fabian Hurzeler ambae ameiongoza Brighton katika michezo mitatu akishinda miwili na sare moja

Kwa upande wa Goli la mwezi limeenda kwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Cole Palmer goli alilofunga dhidi ya Wolves wakati wababe hao wa darajani wakiishindilia Wolves bao 6-2

Save bora ya mwezi imeenda kwa Golikipa wa washika mitutu wa jiji la London Arsenal David Raya, katika mchezo dhidi ya Aston Villa Arsenal ikishinda 2-0 dimbani Villa park

Related Articles

Back to top button