EPL

Marmoush kumpiga tafu Halaand Etihad

MANCHESTER:MANCHESTER City wametangaza rasmi usajili wa mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Eintracht Frankfurt Omar Marmoush ambaye amesaini mkataba wa miaka minne na nusu kukipiga klabuni hapo hadi mwaka 2029.
Marmoush mwenye umri wa miaka 25 anakuwa raia wa kwanza wa Misri kuwahi kucheza klabuni hapo na usajili wake unasitisha tetesi za muda mrefu zilizomhusisha na mabingwa hao watetezi wa ligi kuu ya England.
Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo Marmoush amesema ana furaha sana kutua jijini Manchester na anaamini uwepo wa mwalimu kama Pep Guardiola utamsaidia kuimarika zaidi
“Najisikia vizuri kusaini na moja ya klabu kubwa duniani Manchester City, nimefurahi, familia yangu imefurahi tunajisikia fahari kuwa hapa Manchester. Nataka kushinda makombe na City imekuwa na mafanikio makubwa siku za karibuni, naamini kwa mbinu za Mwalimu kama Pep, miundombinu ya klabu na wachezaji wazuri naamini tutaelekea tunapotaka” – amesema Marmoush
Marmoush alianza soka lake nchini Egypt akiwa na miaka 17 katika klabu ya Wadi Degla kabla ya kuhamia barani Ulaya mwaka 2017 alikozitumikia klabu za Vfl Wolfsburg kabla ya kuhamia Frankfurt ambako amepata mafanikio makubwa akiweka kambani magoli 20 na assist 14 katika michezo 26 ya mashindano yote msimu huu huku msimu uliopita akifunga mabao 17 na apasi 6 za mabao.

Related Articles

Back to top button