Nyumbani

Maofisa michezo kupimwa kwa maendeleo

TABORA: Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro amewaelekeza Maofisa Utamaduni na Michezo  katika ngazi Mkoa, Halmashauri na Wilaya wasimamie urasimishaji wa kazi za sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ukamilifu na wataanza kupimwa utekelezaji kuanzia mwezi Julai, 2024.

Ndumbaro amesema hayo Juni 17, 2024 mkoani Tabora katika kikao maalum na maofisa hao juu ya mpango wa wizara kuanzisha mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana wenye umri  chini ya miaka 20 yatakayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Liberation Cup” na Tamasha la Sanaa “Mwalimu Nyerere Liberation Arts Festival” kwa lengo la kuenzi mchango wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa nchi za Bara la Afrika.

“Kuanzia Julai 1, 2024 katika urasimishaji wa kazi za Utamaduni, Sanaa na Michezo tutaanza kuwapima katika utekekezaji wa jambo hilo,  tutatoa zawadi kwa atakaye fanya vizuri kuanzia wa kwanza hadi wa tatu” amesema Ndumbaro.

Katika hatua nyingine Ndumbaro amewataka maofisa hao watumie fursa ya mashindano hayo yatakayoanzishwa kuibua na kukuza vipaji katika maeneo yao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button