Nyumbani
Yanga inajipigia tu
MBEYA: MABINGWA Watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wameendelea kufanya vizuri kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kukusanya alama tatu muhimu ugenini dhidi ya Ken Gold FC, uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yalifungwa na Ibrahim Bacca dakika ya 13 kwa kichwa ikiwa ni mpira wa faulo uliopigwa na Stephane Aziz Ki.
Hii ni mechi ya pili kwa Yanga kushinda ugenini kwenye Ligi Kuu baada ya kushinda mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya Kagera Sugar.
Baada ya ushindi huo mwembamba, Yanga anasimama nafasi ya 7 akiwa amecheza michezo miwili na kukusanya alama 6.