Mahujaa mguu sawa 2024/25
DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Mashujaa FC, Mohammed Abdallah ‘Bares’, amesema kipindi cha pre season watakuwa na michezo nane ya kirafiki ya kujiandaa na msimu wa 2024/ 25.
Kikosi cha Mashujaa FC tayari imeingia kambini jijini Dar es Salaam na kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Bares ameiambia Spotileo kuwa waliingia kambini jumatatu iliyopita na kufanya mazoezi na baadae wanatarajia kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi.
“Tunatarajia kucheza mechi zisizopungua nane za kirafiki ambazo tutakuwa Dar es Salaam na baadae tutaenda Zanzibar kwa ajili ya kambi fupi na kupata timu za kucheza michezo ya kirafiki,” amesema Bares.
Ameongeza kuwa wanamaiNgizo yasiopungua tisa wote wapo kambini kuendelea na maandalizi kwa kutengeneza timu imara ambayo itafanya vizuri kwa msimu mpya wa ligi.
Bares amesema wamefanya maboresho mazuri kwa kusajili kulingana na mahitaji ya kikosi cjao kulingana na mapungufu yaliyojitokeza kwa msimu ulioisha ambao walicheza kwa presha kubwa katika michezo ya mwisho kutamatika kwa ligi hiyo.