Madonna amlilia kaka yake aliyefariki kwa saratan
NEW YORK: MWANAMUZIKI wa Pop, Madona amemuomboleza kaka yake, Christopher Ciccone, aliyefariki akiwa na miaka 63 kutokana na ugonjwa wa saratani.
Madona amemuomboleza kaka yake huyo ambaye ni mmoja kati ya ndugu zake saba, kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika ujumbe wa maombolezo.
Madona aliandika na pia aliweka picha akiwa na kaka yake huyo huku akiandika kwamba: “Ndugu yangu Christopher hayupo. Alikuwa mtu wa karibu zaidi kwangu kwa muda mrefu. Ni vigumu kueleza uhusiano wetu,
“Lakini ilikua ni kuelewa kuwa tuko tofauti. Tulishikana mikono na kucheza kupitia tabia zetu, tulipokuwa utotoni dansi ilikuwa aina ya gundi iliyotuunganisha pamoja.”
Madonna alikumbuka zaidi jinsi chuo cha ballet kilivyokuwa patakatifu kwake na Christopher, akisema: “Mwalimu wangu wa ballet pia aitwaye Christopher- alitengeneza msingi salama kwa kaka yangu, na tulipokuwa New York alinifuata pia,
“Tulicheza pamoja tulipokuwa Jiji la New York! Tulikula sana na tulicheza muziki kama wanyama wenye njaa na tulicheza pamoja kwenye jukwaa mwanzoni mwa kazi yangu na hatimaye, akawa Mkurugenzi wa Ubunifu, wa ziara nyingi za Papa kiasi kwamba ilibidi ubusu pete yake ili kupata baraka zake,” alieleza Madona.
Madonna alimalizia kwa kueleza kwamba mateso ya kaka yake yalikuwa yameisha, akisema: “Nina furaha kwamba hatateseka tena.. Hakutakuwa na mtu kama yeye. Najua anacheza dansi mahali fulani.”
“Nilijitahidi kumuweka hai kwa muda mrefu iwezekanavyo,” alikiri. “Alikuwa na maumivu makali kuelekea mwisho. Kwa mara nyingine tena, tulishikana mikono. Tulifumba macho na tukacheza. Pamoja.”
Habari hii ya kuhuzunisha ilikuja muda mfupi baada ya kufariki kwa mama yao wa kambo, Joan Clare Ciccone, ambaye alifariki kwa saratani mnamo Septemba 24.