Ligi Daraja La Kwanza

Mabingwa Betika watambiana dabi ya Kariakoo

WAKATI mashabiki, wadau na wapenda soka nchini wakihesabu saa kadhaa kuelekea dabi ya watani wa jadi Simba na Yanga, washindi wa Betika Mtoko wa Kibingwa wametua kuishuhudia dabi hiyo huku wakitambiana kuondoka na pointi tatu.

Simba na Yanga zitakata mzizi wa fitina kesho kwenye uwanja wa Mkapa Dar es Salaam katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika dabi hiyo, mabingwa wa Betika kutoka mikoa mbalimbali nchini wataishuhudia mechi hiyo kwa hadhi ya VIP.

Baadhi ya Mabingwa hao wameizungumzia dabi hiyo baada ya kuwasili jana uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini hapa.

Shomari Makota  wa Lindi ambaye ni mnazi wa Yanga amesema anaamini timu yake itaondoka na pointi tatu akimtaja Prince Dube kung’ara katika mchezo huo.

“Ana historia ya kuifunga Simba, hivyo sina shaka na matokeo ya dabi hii,” ametamba.

Ramadhani Liganga wa Mtwara ambaye ni shabiki wa  Simba amesema hana presha na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Simba lakini anaamini Deborah ataifunga Yanga, kauli sawa na iliyotolewa na Issa Mbonde wa Dodoma aliyemtaja Kibu Denis kumaliza mchezo huo.

Rose Mgala wa Dodoma ambaye ni shabiki wa Yanga amesema Yanga haina mbambamba itashinda mechi hiyo bila presha.

Akizungumza baada ya kuwapokea mabingwa 24 kutoka mikoa ya Mwanza, Dodoma, Mtwara, Tabora, Kagera, Katavi, Mbeya, Morogoro, Arusha, na Mafia, Ofisa Habari wa Betika, Rugambwa Juvenalius amesema washindi hao walishiriki katika kampeni ya Mtoko wa Kibingwa msimu huu.

Amesema katika kampeni hiyo inayofanyika kwa msimu wa nane, washindi 500 waliibuka vinara na kujishindia zawadi mbalimbali ikiwamo kuishuhudia dabi hiyo.

“Katika promosheni ya Mtoko wa Kibingwa ilitakiwa kuweka mkeka wenye mechi 3 au zaidi kwa Sh 1000 na kubeti kwa kupiga kodi hizi. 

“Kulikuwa na zawadi mbalimbali za siku, wiki na mwezi ikiwamo pesa taslimu na fursa ya kuishuhudia laivu dabi ya kesho.

“Mabingwa waliopata tiketi ya kuishuhudia dabi wamegharamiwa tiketi za ndege kwenda na kurudi kutoka mikoani mpaka jijini Dar na kuungana na mabingwa wa Dar es Salaam ambapo Betika imewagharamia Malazi, Chakula, na tiketi za VIP kuishuhudia dabi hiyo uwanjani,” alisema.

Mabingwa hao watawasili uwanja wa taifa kwa msafara wa king’ora kuishuhudia dabi hiyo.

Balozi wa Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa, Baraka Mpenja amesema kabla ya kuishuhudia dabi hiyo mabingwa hao wameshiriki katika bata la Mtoko lililoandaliwa na Betika jana.

Related Articles

Back to top button