Ligi Daraja La Kwanza

Yanga inawaogopesha watu

YANGA imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Ngao ya Jamii baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam FC, kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mchezo huo uliomalizika kwa dakika 90 kwa Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 4-1, mabao ya Yanga yakifungwa na Clement Mzize dakika ya 92, Stephane Aziz Ki ameipatia bao la tatu dakika ya 30, Chadrack Boka dakika ya 28,na Prince Dube dakika ya 19.

Bao la Azam FC limefungwa dakika ya 13, kupitia mchezaji wake Feisal Salum ‘Fei Toto ‘.

Kwa ushindi huo Yanga inatawazwa ubingwa wa wa Ngao ya Jamii 2024/25 wakimpokea Simba, watetezi wa kombe hili kwa msimu uliopita ambaye amemaliza nafasi ya tatu huku Azam FC akiwa nafasi ya pili.

 

 

 

Related Articles

Back to top button