Nyumbani

Mabadiliko katika wizara

DAR ES SALAAM: BAADA ya miezi minne, Rais Samia Suluhu Hassan alifanya mabadiliko madogo tena katika Baraza lake la Mawaziri na miongoni mwa wizara zilizoguswa ni Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Awali, ilikuwa inatambulika kama Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lakini baadaye neno Habari likatolewa na kupelekwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Dk Damas Ndumbaro ni miongoni mwa mawaziri walioongoza kusimamia wizara nyingi tangu Rais Samia aingie madarakani Machi 19, 2021.

Dk Ndumbaro, ambaye alianzia Wizara ya Katiba na Sheria, kisha Maliasili na Utalii; na baadaye Michezo, Sanaa na Utamaduni hivi karibuni alirejeshwa tena Wizara ya Katiba na Sheria.

Awali, Ndumbaro aliingia wizara hiyo kuchukua nafasi ya Dk Pindi Chana ambaye kwa sasa yupo Wizara ya Maliasili na Utalii.

Jerry Silaa, aliyewahi kuhudumu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na sasa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, naye aliguswa katika mabadiliko hayo.

Sekta ya Habari ambayo ilikuwa sehemu ya wizara anayosimamia Silaa, imerejeshwa ilikokuwa wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Samia pia ameunda Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, sekta hiyo ikiondolewa kutoka iliyokuwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

Katika hilo, Rais Samia alimteua Profesa Palamagamba Kabudi, kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Profesa Kabudi alirejeshwa kwenye uwaziri Agosti 14 mwaka huu na kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.

Naibu Waziri Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ aliyeteuliwa kama Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo baada ya Habari kurejeshwa ataendelea kusalia katika nafasi hiyo.

Gerson Msigwa, alirudishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, lakini akiongezwa jukumu lingine la kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.

Related Articles

Back to top button