Ligi KuuNyumbani

Yanga yazindua kampeni Ligi Kuu leo

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Yanga leo inaanza kampeni ya kutetea taji hilo dhidi KMC.

Mchezo huo pekee wa ligi hiyo leo utafanyika uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.

Takwimu zinaonesha Yanga na KMC zimekutana mara kumi, mabingwa hao watetezi wakishinda mara saba, sare mara mbili na kupoteza mchezo mmoja.

Patashika wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Singida Fountain Gate na Tanzania Prisons, Agosti 22, 2023.

Katika mchezo pekee wa Ligi Kuu uliopigwa Agosti 22, wenyeji Singida Fountain Gate imelazimishwa suluhu na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa CCM Liti mjini Singida.

Related Articles

Back to top button