
LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa viwanja tofauti Dar es Salaam.
Azam itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting katika uwanja wa Azam Complex wakati Dodoma Jiji ni wageni wa KMC katika uwanja wa Uhuru.
Azam inashika nafasi ya 2 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 21 baada ya michezo 10 wakati Ruvu ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 11.
KMC ipo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 14 baada ya michezo 11 wakati Dodoma jiji inayosuasua ipo nafasi 15 ikiwa na pointi 6 baada ya michezo 10.