LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili mkoani Kagera na Dar es Salaam.
Mashujaa inayoshika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 10 baada ya michezo 15 itakuwa mgeni wa Kagera Sugar iliyopo nafasi ya 10 ikikusanya pointi 17 kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.
Katika michezo mitano ya mwisho, Mashujaa haijashinda hata mchezo mmoja, imetoka sare 2 na kupoteza 3.
Mkoani Dar es Salaam, Azam inayoshika nafasi ya 3 ikiwa na pointi 32 baada ya michezo 14 itashuka kwenye uwanja wake wa Azam Complex kuikaribisha Geita Gold iliyopo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 16.
Yanga inaongoza Ligi Kuu ikiwa na pointi 40 baada ya michezo 15 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 36 kwa idadi hiyo hiyo ya michezo.