Leonardo DiCaprio akwama kwa Vittoria Ceretti

NEW YORK: MUIGIZAJI aliyetamba katika filamu ya Blood Diamond, Leonardo DiCaprio ameshangaza wengi baada ya kuendelea na mpenzi wake wa sasa Vittoria Ceretti licha ya kuvuka miaka 25.
Tabia ya kushangaza ya DiCaprio ambayo inachukiza wadau wengi wa masuala ya mahusiano ni kwamba huwa na tabia ya kuachana na wachumba zake pindi tu wanapotimiza miaka 25 lakini imekuwa tofauti kwa mwanamitindo Vittoria Ceretti mwenye umri wa miaka 26, ambaye anakaribia kufika miaka 27.
Kwa miaka mingi, historia ya uchumba ya DiCaprio imefuata mtindo wa ‘chini ya miaka 25’ hadi wakamtungia vijana nchini humo wakamuita mtu mwenye sheria zake ‘Leo’s Law’. Alikuwa kwenye uhusiano na Bar Refaeli hadi 2010, mwaka ambao alifikisha miaka 25.
Vivyo hivyo, mapenzi yake na Kelly Rohrbach yaliisha mnamo 2015, alipofikia umri huo wa miaka 25.
Nina Agdal, muigizaji mrembo alichumbiana na mwigizaji huyo kutoka 2016 hadi 2017 mwaka huo huo alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 25 naye ikawa hivyo hivyo walitengana.
Ndipo nyota huyo wa ‘Catch Me if You Can’ na mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 26 ukaanza mwanzo mpya wa mapenzi yao lakini msichana huyo mwaka huu ametimiza miaka 26 na hivi karibuni atatimiza miaka 27 lakini uhusiano wao upon a nguvu mno tofauti na wenzake waliopita.
Mwanamitindo huyo anasema hana uharaka wa ndoa kwa sasa kwa sababu alishawahi kuolewa na DJ wa Kiitaliano anayefanyia shughuli zake nchini Marekani, Matteo Milleri.