
LOS ANGELES: MWIMBAJI wa Pop Taylor Swift amekuwa na mabadiliko makubwa katika maisha yake akiwa na umri wa miaka 35, huku akipanga kuhamia Nashville badala ya Los Angeles au New York ili kuwa karibu na jiji la Kansas anakotoka mpenzi wake, Travis Kelce.
Vyanzo vya habari vimeeleza kwamba uamuzi wa kuhamia Nashville, kwa msanii huyo kunaashiria hamu ya Taylor ya maisha bora zaidi katika jiji hilo na kujitolea kwa mpenzi wake huyo huku wakiweka mipango ya maisha ya muda mrefu.
Msingi wa Nashville unawafaa wanandoa hao, kwa kuwa Swift tayari anamiliki shamba lenye thamani yad dola milioni 2.5.
Sio tu kuwa karibu na Kansas City, lakini Taylor sasa atakuwa na Travis kwa urahisi wakati wa msimu wa NFL, na pia kwa sababu ya mama yake, kupenda kuwa Nashville, usalama na haiba ya mahali hapo inaonekana kuleta mabadiliko yote kwa Taylor.
Awali nyumba ya mpenzi wa mwanamuziki huyo yenye thamani ya dola milioni 6 iliyopo Kansas City ilivamiwa na kuibiwa mali nyingi lakini baada ya tangazo la kuhamia huko imeongeza mvuto zaidi na hata thamani ya nyumba za Nashville zimeongezeka.
Kwa kuzingatia wizi huo, usalama umeimarishwa katika makazi ya Kelce, lakini huenda wenzi hao wakahisi salama zaidi katika jumba la kifahari la Swift Nashville, ambalo huwapa faragha na usalama wanaohitaji. Ingawa wanandoa hao wanaishi maisha ya kushtukiza na msimu wa NFL na kazi ya muziki inayoendelea ya Swift.
Kwa kuwa Nashville itakuwa kimbilio lake salama, yeye na Kelce inaonekana wanashughulikia mambo muhimu ya maisha yao ya kibinafsi na ya kikazi. Kwa hivyo ni wazi kuwa wawili hawa wako makini sana hivi kwamba inaonekana Nashville itakuwa sehemu kuu ya maisha yao katika siku za usoni.