Talaka ya Brad Pitt, Angelina Jolie yatoka kwa siri

NEW YORK: NYOTA wa Hollywood Brad Pitt ameonekana akiendelea na shughuli zake huku akiwa na furaha baada ya Sakata la talaka yake kutoka kwa aliyekuwa mke wake Angelina Jolie kukamilika.
Kulingana na ripoti ya jarida la People talaka hiyo imetoka tangu Desemba mwaka jana.
Muigizaji huyo mwenye miaka 61, ambaye hivi karibuni ataonekana katika filamu ijayo na Jolie walitatua rasmi talaka yao mnamo Desemba 2024, na kumaliza mzozo wao wa muda mrefu wa kisheria uliochukua miaka minane.
“Brad Pitt ana furaha kwamba talaka iko nyuma yake,” chanzo kiliambia chapisho hilo, na kuongeza, “Mambo hayo yamefanyika kwa siri ya familia.”
Mdau huyo wa ndani pia alibaini kuwa Brad ana furaha katika uhusiano wake mpya na mbunifu wa vito Ines de Ramon, ambaye wamechumbiana tangu mwishoni mwa mwaka 2022.