Coletha awapa mchongo wasanii
Msanii wa Filamu nchini ambaye pia ni mfanyabishara, Coletha Raymond amewataka wasanii kujiwekeza kimaisha tofauti na kazi zao walizoeleka nazo ili kujikwamua na maisha yao ya baadae.
Amesema wasanii hawana kazi zao binafsi wanazo jivunia na baadala yake kila siku wanasema wao ni wakubwa na kusahau umaarufu wao hautoshi wanapaswa kuwa na vitu vya kujivunia kwenye maisha .
Coletha ameiambia Spoti Leo kuwa wasanii wengi bado hawajawekeza huwa wanategemea malipo ya kwenye kazi za sanaa ndio maana baada ya sanaa wanakuwa tegemezi kwa jamii hata wanapofikwa na matatizo.
“Yaani hii kazi ndio maana mdogo wangu Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alijiamulia kujifungulia Mgahawa wake, mapema tofauti na Sanaa anazozifanya amejiongeza kafungua Shishi Food.
“Sasa ni mpishi mkubwa asipo kuwa na kuigiza utamkuta ofisini, wasanii wenye biashara zao na kazi zao mjini wanahesabika ,”amesema.