Kwa mnaomtaka,anauzwa

MANCHESTER:Televisheni ya Skysports imeripoti kuwa mabingwa wa zamani wa Ligi kuu ya England Manchester united hawana pesa za kutosha kufanya usajili wa wachezaji wapya dirisha la Januari 2025 hivyo inapanga kuwapiga bei nyota kadhaa akiwemo mshambuliaji wa klabu hiyo Marcus Rashford.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa wawekezaji wa klabu hiyo kampuni ya INEOS inatafuta pesa kukiboresha kikosi cha mashetani wekundu na wako tayari kumpiga mnada Rashford lakini hadi sasa hakuna klabu iliyoonesha nia ya kumsajili.
Inaelezwa kuwa mawazo hayo ya kumuuza Rashford huenda yakabadilika kutokana na kuongezeka kwa ‘form’ yake ya uchezaji chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Ruben Amorim.
Rashford alieanza soka la kulipwa miaka 9 iliyopita amefunga mabao 3 katika mechi 5 tangu kutua kwa kocha Amorim klabuni hapo. Na kocha huyo ameapa kumsaidia kurejesha kiwango chake.