Liverpool kumkosa Allison kwa wiki 6
LIVERPOOL:Mlinda lango wa majogoo wa jiji la Liverpool Alisson Becker amepata jeraha la msuli wa paja, jeraha ambalo litamfanya golikipa huyo namba moja wa Liverpool kutoonekana uwanjani kwa takribani muda wa wiki 6, angalau hadi baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa ya mwezi Novemba.
Allison mwenye miaka 32 alitolewa katika kipindi cha pili cha mchezo wa wikiendi iliyopita Liverpool ikishinda 1-0 dhidi ya Crystal Palace, licha ya kupatiwa matibabu uwanjani kabla.
Akizungumza baada ya mchezo huo, kocha mkuu wa Liverpool Arne Slot alionesha mashaka ya kuwa na mchezaji huyo muhimu wa Liverpool katika siku za karibuni.
Allison Becker Anatarajiwa kukosa mechi 7 zikiwemo zile muhimu dhidi ya Chelsea, Arsenal, Brighton na Aston Villa kwenye Ligi Kuu ya England, pamoja na mechi mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya RB Leipzig na Bayer Leverkusen.
Kutokana na kukosekana kwa golikipa huyo, itamlazimu Arne Slot kumtumia Caoimhin Kelleher au Vitezslav Jaros, lakini ni wazi kuwa Kelleher ndiye golikipa namba mbili wa Liverpool.
Ikumbukwe pia Liverpool ilimsaini golikipa wa Georgia anayekipiga Valencia, Giorgi Mamardashvili ambaye atajiunga na majogoo mwishoni mwa msimu huu.