EPLKwingineko

Newcastle yamsajili Kuol

KLABU ya Newcastle United ‘The Magpies’ imekubali dili la kumsajili kinda wa Kimataifa wa Australia, Garang Kuol mwenye umri wa miaka 18 kutoka Central Coast Mariners.

Atajiunga na The Magpies Januari, 2023.

Ripoti zimesema Newcastle imelipa pauni 300,000 sawa na shilingi 761,303,220 za awali kabla ya vifungu vya nyongeza.

“Ligi Kuu Uingereza ni jambo kubwa kila mmoja anaangalia lakini hakuna mtu anayefikria kuwa atafikia urefu huo. Kuwa mmoja wa watu hao, kuwa katika nafasi niliyopo, inashangaza,” amesema Kuol.

Kocha wa Newcastle Eddie Howe amesema Kuol ni mchezaji mwenye kipaji cha mbinu nyingi za mchezo.

“Ni mwepesi, mwenye mbio na mmaliziaji mzuri,”amesema Howe.

Kuol amejiunga na Newscastle wiki moja tu baada ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kucheza timu ya taifa ya Australia tangu Harry Kewell aliyekuwa na miaka 17 mwaka 1996.

Kuol aliyezaliwa Misri aliwasili Australia pamoja familia yake wakiwa wakimbizi wakitokea Sudan Kusini.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button