EPL

Kudus yamemkuta

LONDON:Chama cha soka nchini England (FA) kimemuongezea Winga wa West Ham united Mohammed Kudus adhabu inayotokana na kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo wa ligi ya kuu ya England dhidi ya Tottenham Hotspur mchezo uliopigwa tarehe 19 mwezi Oktoba mwaka huu kutoka kukosa mechi 3 na sasa atakosa 5.

Katika mchezo huo Kudus alicheza ‘foul’ kwa beki wa kati wa Spurs Micky van de Ven mnamo dakika ya 83 jambo lililozua tafrani, beki huyo mholanzi akidai Kudus alimtwanga ngumi usoni.

Kudus alipewa kadi ya njano kwa tukio hilo kabla ya mwamuzi Andy Madley kubadilisha maamuzi yake na kumpa kadi nyekundu baada ya tukio hilo kupitiwa upya na waamuzi wa VAR walioamua Kudus alicheza mchezo hatari kwa Van de Ven, kadi ambayo iliyomfanya akose mechi 3 na sasa atakosa mechi mbili zaidi.

Winga huyo tayari mekosa mechi dhidi ya Manchester United, Nottingham forest na alikua akimaliza adhabu hiyo wikiendi hii dhidi ya Everton lakini sasa ongezeko la adhabu hii litamfanya kukosa mechi dhidi ya Newcastle Novemba 25 na Arsenal Novemba 30.

Related Articles

Back to top button