PSG yamsaka Rashford, Diaz
PARIS Saint Germain wanaandaa dau la pauni milioni 80 kumnunua mshambuliaji wa Manchester United, Muingereza Marcus Rashford, 26 na watakuwa tayari kumlipa pauni 500,000 kwa wiki, mtandao wa Star umeripoti.
Julai 18, 2023 Manchester United ilimpa Rashford mkataba wa miaka mitano ambapo hadi sasa ameshatumikiwa mwaka mmoja na mkataba huo utaisha Juni 30, 2028.
Imeripotiwa pia klabu hiyo inavutiwa na winga wa Liverpool kutoka Colombia Luis Diaz, 27, kama mbadala wa Kylian Mbappe, 25, ambaye anatazamiwa kujiunga na Real Madrid, taarifa hiyo kwa mujibu wa El Pais – in Spanish
Kwa upande wa Luis Diaz aliyejiunga na Liverpool akitokea FC Porto Januari 31, 2022 alisaini mkataba wa miaka mitano.
PSG inapanga kuboresha kikosi chake kuelekea msimu ujao baada ya kutokuwa na uhakika wa kubaki na Kylian Mbappe.