EPL

Amorim kimeeleweka

MANCHESTER: Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya England Manchester United wanatarajia kumtangaza Ruben Amorim kama meneja mpya wa kikosi hicho muda wowote leo Alhamisi.

Kwa mujibu wa gazeti la The Athletic Amorim mwenye miaka 39 atasalia na klabu yake ya Sporting Lisbon angalau hadi mapumziko yajayo ya michezo ya kimataifa.

Tayari klabu ya Sporting Lisbon imethibitisha biashara na United kupitia soko la hisa la Lisbon kuwa na biashara na wababe hao wa jiji la Manchester.

Kituo cha Sky Sports cha nchini England kimefichua kuwa United inataka kuharakisha mchakato wa kumpata meneja huyo na imeongeza Euro Milioni moja kwenye milioni kumi ya awali ili meneja huyo awahi kuwasili klabuni hapo.

Mapema Jumatatu United ilimfuta kazi meneja wake Erik Ten Hag aliyedumu kwa miaka miwili baada ya kipigo cha 2-1 kutoka kwa WestHam united na kusalia nafasi ya 14 kunako msimamo wa ligi hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button