Kompany ataka makali Bayern
MUNICH. Kocha mpya wa the Bavarians Bayern Munich Vincent Kompany ametaja vipaumbele vyake huku akiwataka wachezaji klabuni hapo kujituma kwa ajili ya klabu
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Kompany amesema kwamba yeye ni kocha mkali hivyo atakuwa mkali kuhakikisha klabu hiyo inafikia malengo ya kumuajiri.
“Nataka wachezaji wa Bayern Munich wawe majasiri mchezoni. Kiasili mimi ni mkali hivyo nataka timu iwe kali, nataka wawe na maamuzi wanapokuwa uwanjani nataka kuona ujasiri wao uwanjani nataka wawe na ari kila dakika ya mchezo, muda wote.
Vincent Kompany ambaye atakutana tena na wachezaji aliowahi kucheza nao ligi moja kama Harry Kane na mchezaji mwenzake wa zamani wa Mancheter City Leroy Sane ambaye Sasa watakutana kama mwalimu na mwanafunzi.