Bundesliga
Neuer karudi!

MUNICH: GOLIKIPA namba moja wa Bayern Munich Manuel Neuer atarejea kwenye milingoti mitatu katika mchezo wa Bundesliga kesho Jumamosi dhidi ya Borussia Monchengladbach baada ya kuwa nje ya uwanja baada ya kupata jeraha la mbavu.
Neuer alipata jeraha hilo katika mchezo wa Bundesliga dhidi ya Bayer Leverkusen uliopigwa Desemba 3 mwaka jana. Mchezo ambao pia ulichafua rekodi yake ya kadi, akipata kadi yake ya kwanza nyekundu katika maisha yake ya soka.
Kocha wa Bayern Vincent Kompany amethibitisha kurejea kwa nguli huyo huku akisema pia kiungo mshambuliaji wake Jamal Musiala ataukosa mchezo huo kutokana na kuugua mafua.