Habari Mpya

Ntibazonkiza aitabiria makubwa Yanga

KIUNGO mshambuliaji wa Geita Gold, Saido Ntibazonkiza ameitabiria makubwa timu yake ya zamani Yanga akisema sasa imekuwa bora.

Akizungumza na Spotileo, mchezaji huyo ameaema matokeo mazuri wanayoyapata hivi sasa ni kutokana na kikosi hicho kuimarika zaidi.

“Nimeangalia mechi zao nyingi za Yanga, wameimarika, wachezaji waliowaongeza wana viwango vya juu ndio maana nasema wataendelea kufanya vizuri msimu huu,” amesema Ntibazonkiza.

Amemmwagia sifa mshambuliaji Fiston Mayele akisema ni mtu hatari anapokuwa mbele ya lango la mpinzani na ataendelea kufunga kutokana na kuzungukwa na wachezaji wengi hodari.

Related Articles

Back to top button