Kwingineko

Kipute marudiano nusu fainali UEL, UECL

MICHEZO mitatu ya marudiano ya michuano ya Ligi za Europa na Conference barani Ulaya inafanyika leo kwenye viwanja tofauti.

Katika Ligi ya Europa, Atalanta itakuwa uwanja wa nyumbani kuikaribisha Marseille wakati Roma ni mgeni wa Bayer Leverkusen.

Marseille na Atalanta ziligawana pointi kwa sare ya bao 1-1 Mei 2 wakati Bayer Leverkusen ilishinda ugegeni dhidi ya Roma kwa mabao 2-0.

Olympiacos itakuwa mwenyeji wa Aston Villa katika mchezo wa Ligi ya Europa Conference.

Katika mchezo wa kwanza Mei 2, Aston Villa ikicheza nyumbani ilikubali kipigo cha mabao 4-2 dhidi Olympiacos.

Related Articles

Back to top button