Kwingineko
Ni vita robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya

MECHI mbili za kwanza za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zinapigwa leo.
Mchezo kivutio utakuwa jijini Manchester, England wakati Manchester City itakapoikaribisha Bayern Munich kwenye uwanja wa Etihad.
Katika kipute kingine Inter Milan itakuwa ugegeni kuivaa Benfica kwenye uwanja wa Luz katika jiji la Lisbon, Ureno.