Ligi Kuu

Kipigo dhidi ya Azam Aussems atajwa

DAR ES SALAAM: ALIYEKUWA Kocha wa Singida Black Stars, Patrick Aussems ametajwa kuwa sababu ya wachezaji wa timu hiyo kutoonesha kiwango kizuri kipindi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.

Singida Black Stars juzi jana usiku ilikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini ukiwa ni mchezo wa nne mfululizo kutopata matokeo mazuri.

Kaimu Kocha wa Singida, Ramadhani Nsanzurwimo amesema kipindi cha kwanza hawakucheza vizuri kwa sababu ya saikolojia ya wachezaji wao kutokubali haraka mabadiliko ya benchi la ufundi.

“Sijafurahiswa jinsi tulivyocheza kipindi cha kwanz, hii inatokea pale inapokuja mabadiliko ya benchi la ufundi, hatuwezi kujua kocha Aussems alikuwa akiishi vipi na wachezaji.

Tulipoenda mapumziko nikazungumza na wachezaji wangu na kuwaeleza mapungufu ya Azam FC kipindi cha pili tukabadilika na kucheza vizuri,” amesema.

Nsanzurwimo amesema wanarudi uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu yake kubwa ikiwemo suala la saikolojia ya wachezaji wao ili mechi zijazo kufanya vizuri na kufikia malengo.

 

Related Articles

Back to top button